Elisa's blog

Pombe kupita kiasi

Drunk in Fisi: Picha: Elisa JosephDrunk in Fisi: Picha: Elisa JosephPombe kupita kiasi ni mbaya. Hebu angalia huyu mtu amepoteza fahamu na amelala bila yeye kujitambua katika Uwanja wa Fisi. Sisi tulijua ameshakufa na tulishindwa kumsaidia au kumshika kwa sababu tuliogopa tutashtakiwa baadaye. Kumbe, kesho yake tulisikia kwamba baada ya masaa kadhaa aliamka na kuweza kuondoka mwenyewe. Yeye ni mwuza machungwa sokoni ya Tandale na akishauza anakuja kulewa moja kwa moja.

Maswali na majibu baada ya filamu Aprili 6 | Q&A after film show

Q: Nani alikushawishi kutengeneza filamu?

Elisa. Sikushawishiwa. Ilikuwa moja ya lengo langu ili latizo kuiokowa jamii. Filamu ina ukweli. Nina lengo la kutengeneza filam ndefu (kuhusu maisha yangu).

Q: Baba yako alikufukuza kwa mara ya kwanza ukiwa na uri gani?

Elisa. Baba yangu alinikataa tangu nikiwa tumboni. Baadae tena. wakati natembea, sijui nilikuwa na umri gani. Mama aliuguwa kichaa wakati huo.

Q: Unasema unajisikia kama si mwathirika lakini furaha yako hasa ni kukutana na baba yako. Je ulikutana nae?

Ujasiri | Courage

Vijana wengi wamependa ujasiri wangu kwa kueleza historia yangu kuhusu maisha yangu ndani ya Virusi vya Ukimwi. Wengi wamesema bora kubadili tabia kwa kupima afya zao.

Wamefurahi sana kuona mimi nikiwa muwazi juu ya masuala ya jamii na Vijana hao wamependekeza nianzishe kikundi (‘camp’)

Mashirika yako wapi? | Where are these NGOs?

Baada ya onyesho la filamu jana, tulipoeka barua kutoka mwanamke mmoja anayeishi Uwanja wa Fisi. Alikuwa amemwomba Hadija kumwandikia, mwenyewe hawezi.

"NI MSICHANA AMBAYO ANAOMBA MSAADA KUTOKA KWENU

Mtoto abakwa Uwanja wa Fisi | Another child raped at Hyena Square

Jana tarehe 30 Machi nilikuwa nikipitapita pale uwanja wa fisi nikasikia vijana wakisemasema kuwa kuna mwenzao aliyemchukua mtoto mdogo akaenda naye.

Mtoto huyo alimwelezea kuwa alifukuzwa kule anakofanyia kazi za ndani alipofukuzwa akawa anahangaika huku na huko mara akaibukia uwanja wa fisi akakutana na huyo kijana ambaye alimwelezea matatizo yake. Huyo kijana akamuuliza anatokea wapi mtoto akamjibu kuwa anatokea Singida. Hapo akamwambia kuwa yeye ni kaka yake kwa hivyo akaenda naye hadi kwake.


Theme & Icons by N.Design Studio
© 2007 Maweni Farm
Syndicate content